KABLA YA KUJENGA ZINGATIA HAYA
Kwa kawaida ukifikiria kujenga huwa huwazi juu ya hali ya hewa na wala hufikirii kuhusu nyenzo / materials za ujenzi kama zitakuwa kikwazo katika ujenzi wako.Katika tovuti hii tumekuwa tukikuletea makala mbalimbali za ujenzi ili kukufumbua macho zaidi na kurahisisha shughuli ya ujenzi kwako.Ikiwa unafikiria kuanza kujenga ni vyema ukazingatia mambo haya saba ( 7 ) muhimu ili kufanikisha zoezi la ujenzi kwenda sawia.
1.FEDHAKabla ya kuanza ujenzi hakikisha una chanzo kizuri cha mapato ambacho kitakurahisishia shughuli ya ujenzi hivyo kukamilisha nyumba yako kwa wakati.Pia ni vyema kuwa makini na matumizi ya fedha katika kila hatua ya ujenzi kwani waweza tumia kiasikikubwa cha fedha bila sababu ya msingi hivyo kujikuta unaishia njiani
.2.MICHOROArchitectural DrawingsVIEW SLIDE SHOWDOWNLOAD ALLUkiwa tayari una kiwanja chako basi yakupasa kutafuta msanifu majengo (Architect) ambaye atakamilisha suala lote la ujenzi na kukupa ushauri wa kitaalamu kulingana na mahitaji yako unayoyataka.Ili upate kufahamu michoro inayotakiwa ili upate kibali cha ujenzi ingiahapaIli upate kufahamu orodha ya watu wanaohitajika kukamilisha ujenzi wako ingiahapa.Wakati wa kubuni ramani yako ni vyema kuwa makini ili upate ramani inayoendana na mtindo wa maisha yako ya kila siku.
3.SHERIA , TARATIBU NA KANUNIUnapaswa kubaini kuwa si kila kiwanja kinafaa kulingana na mahitaji yako , Huenda wewe unahitaji nyumba ya kawaida tu lakini sheria za mahali kiwanja chako kilipo inataka pajengwe nyumba za ghorofa moja.Hivyo waweza kujikuta matatizoni na kushindwa kumaliza ujenzi wako katika muda stahiki. Ni vizuri kuepuka kununua viwanja ambavyo hujui taratibu namalengo ya viwanja husika , kama ni kwa shughuli za makazi au viwanda.Kumbuka ukizingatia mlolongo huu basi ujenzi kwako utakuwa rahisi mno.
4.MAKADIRIOIli uweze kupata picha ya karibu kabisa ni kiasi gani waweza kutumia kufanikisha ujenzi wako unapaswakupata makadirio katika kila nyanja ya taaluma itakayo husika. Baadhi ya vipengele vya kuzingatia ili kupata makadirio ni –:( a ) Ujenzi wa nyumba husika( b) Gharama ya kutandaza nyaya za umeme ( Wiring) , n.kIli kurahisha shughuli hii ya ukadiriaji wa gharama nivyema ukaonana na mkadiriaji gharama ( Quantity Surveyor ) ili aweze kufanya kazi hii kwa ufanisi mkubwa
.5.BIMA YA NYUMBA (HIYARI)Ili kuepuka kurudi nyuma pindi inapotokea kuzuka kwa moto au majambazi kuvamia eneo lako la ujenzi na kuleta maafa ni vyema ukakata bima ya nyumba yako ili uweze kufidiwa ukikumbwa na majanga kama hayo,
6.KIBALI CHA UJENZIBaada ya kujiridhisha na gharama za makadirio ya gharama za ujenzi basi waweza songa mbele na kupeleka michoro yako katika mamlaka husika ( manispaa ya mji / jiji ) ili waweze kushughulikia utoaji wa Kibali cha Ujenzi.Punde upatapo kibali chako utapewa na masharti mbalimbali yatayo tamalaki ujenzi wako
.7.JIANDAE NA UJENZIPindi unapokuwa unasubiri kibali kutoka manispaa , waweza kuanza mazungumzo na kampuni za ujenzi( makandarasi ) mbalimbali ili uweze kuratibu mtirirko wa shughuli ya ujenzi wa nyumba yako.
Comments
Post a Comment